Uundaji Wa Maneno
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
 • 0 Votes - 0 Average
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4
 • 5
Uundaji Wa Maneno
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 116 in 77 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,933.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Uundaji Wa Maneno

0
0
Utangulizi
Uundaji wa maneno ni kitendo cha kuzalisha maneno mapya kunakotokana na sababu mbalimbali ili kukidhi mahitaji yaliyopo katika jamii.
Pia maneno mapya huundwa kutokana na mabadiliko yanayoikumba jamii kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni, kisayansi na teknolojia.
 NJIA ZA UUNDAJI WA MANENO
Kuna aina mbili za uundaji wa maneno
 (a) Uambishaji
(b) Mnyumbuliko
 1. UAMBISHAJI

Ni kitendo cha kuongeza viambishi mwanzoni na mwishoni mwa mzizi wa neno.
Kwa mfano: Cheza -  anachezewa, anachezea,mchezo na wachezaji
                     Pika     - wanapikiwa, anapika
Viambishi ni mofimu zinazoongezwa kabla au baada ya mzizi wa neno
Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha kiisimu chenye muundo wa kisarufi.
Mzizi ni sehemu ya neno ambayo haibadiliki ukiondoa viambishi vilivyoko mwanzoni na mwishoni mwa neno.
Kuna aina mbili za viambishi
 1. Viambishi awali
 2. Viambishi tegemezi

 
 
 1. Viambishi awali

Ni mofimu zinazoongezwa mwanzoni mwa mzizi wa neno kwenye uambishaji, kwa mfano;
Mzizi Lima – analima, atalima, walilima, wanalima.
 
 
Dhima za viambishi awali
 • Kudokeza/ kuonyesha nafsi,kwa mfano; Anacheza (Nafsi ya 3 Umoja)
                              Wanacheza( Nafsi ya 3 wingi)
                              Unacheza( Nafsi ya 2 Umoja)
                               Mnacheza( Nafsi ya 2 wingi)
 • Hudokeza idadi ya umoja na wingi,kwa mfano;Anacheza – Idadi(umoja)
                  Wanacheza- Idadi(wingi)
 • Hudokeza njeo(wakati), kwa mfano; Analima – wakati uliopo       Atalima – wakati ujao
                                                           Alilima – wakati uliopita
 • Hudokeza hali mbalimbali,*hali ya masharti kwa mfano; Akija
                                                Ukifika
*Hali ya kuendelea kwa jambo, kwa mfano; Anaeleza
                                                                      Anakula
                *Hali timilifu, kwa mfano; Ameenda
                                                           Amesoma
                                                           Amecheza
 • Hufanya kazi ya kuonyesha urejesho wa mtenda, mtendwa na mtendewa   Kwa mfano; Alipompiga
                        *po -urejeshi wa mtenda
                         *m -urejeshi wa mtendwa
 • Hudokeza uyakinishi na ukanushi, Kwa mfano; Anaimba- haimbi                                                                            Uyakinishi- ukanushi
 • Huonyesha mzizi wa neno,Kwa mfano; Anacheza- chez (mzizi)
                    Anapika – pik (mzizi wa neno)
 1. Viambishi Tamati

Ni mofimu ambazo huongezwa mwishoni mwa mzizi wa neno
Kwa mfano; Lima- limika,limisha,limwa
Lim- Mzizi wa neno
Dhima za viambishi tamati
 • Hufanya kazi ya kuzalisha kauli mbalimbali,
Mfano; Kauli ya mtenda
                             lima,cheza, imba
              Kauli ya mtendewa
                             Limwa
                             Chezwa
                             Imbwa
               Kauli ya kutendwa
                                Limia
                                Chezea
                                Imbia
               Kauli ya kutendeka
                                 Limika
                                 Chezeka
                                 Imbika
               Kauli ya kutendewa
                                Limiwa
                                Chezesha
                                Imbiwa
 1. MNYUMBULIKO

Ni kitendo cha kuongeza viambishi mwishoni mwa mzizi wa neno, kwa mfano; cheza, chezewa, chezesha,chezeshana, chezeshewa.
Mnyumbuliko huweza kujitokeza katika vipengele vifuatavyo,
kwa mfano;*Kitenzi- Pigana, pigwa, pigiana
                   *Nomino;- Nyumba- nyumbani,
                                      Shule- shuleni
 
Dhima za mnyumbuliko
 • Hurefusha maneno,
Kwa mfano; Piga, pigwa, pigana,
                    Cheza, chezewa, chezesha
 • Huzalisha maneno mapya
Kwa mfano;Bora-Boresha
                    Weka- wekeza
 • Hupanua maana ya neno
Kwa mfano; Pigisha-kutanisha vitu kwa nguvu
                     Pigia- 1.Piga kwa niaba ya mtu Fulani
                                2.Piga kwa kutumia kifaa Fulani
 
MOFIMU
Ni neno au sehemu ya neno yenye maana maalumu kisarufi, kwa mfano; mama, baba, mtoto.
Kuna aina mbili za mofimu;
 1. Mofimu huru
 2. Mofimu tegemezi

 
Mofimu Huru
Ni aina ya mofimu ambayo hujengwa na maneno yaliyo na maana kamili na ambayo hayagawanyiki katika sehemu ndogo, kama yatagawanyika zaidi hupoteza maana. Kwa mfano; Asha, maziwa, Tanzania, mapinduzi
 
Mofimu Tegemezi
          Ni aina ya mofimu ambayo ni sehemu ndogo ya neno yenye maana kisarufi na haiwezi kusimama peke yake na kuleta maana ya kisarufi na haiwezi kusimama peke yake na kuleta maana lakini inaweza kugawanyika katika sehemu ndogo ya neno yenye maana kisarufi
Kwa mfano; a_na_li_ma
“a” huonyesha nafsi

Dhima za Mofimu
 • Huonyesha nafsi, kwa mfano; anacheza- huonyesha nafsi ya tatu umoja
 • Huonyesha wakati (njeo), kwa mfano; anacheza- huonyesha wakati uliopo
 • Huonyesha ukanushi,Kwa mfano; Hajacheza- hukanusha
 • Huonyesha kauli mbalimbali,
kwa mfano; Piga- kutenda
                    Pigwa- kutendewa
                     Pigana- kutendeana
 • Huonyesha urejeshi wa mtenda/mtendwa
Kwa mfano; walimcheza- urejeshi wa mtenda

 

 
(This post was last modified: 12-04-2017 05:00 PM by MyElimu.)
12-04-2017 02:22 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
Post Icon Aina Za Maneno MyElimu 0 5,989 10-19-2017 06:54 PM
Last Post: MyElimuUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)