Usimulizi
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
 • 0 Votes - 0 Average
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4
 • 5
Usimulizi
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 111 in 73 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,931.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Usimulizi

0
0
Maana ya Usimulizi
Ni dhana inayoelezea utoaji wa habari au hadithi kwa kutumia mdomo au maandishi.
Pia usimulizi huweza kuwa wa matukio mbalimbali kwa kuzingatia ufasaha wa Kiswahili yaani kiimbo, matamshi, sarufi na matumizi ya lugha
Aina za Usimulizi
(a).Usimulizi wa hadith
(b)Usimulizi wa habari

Usimulizi wa Hadithi
Ni masimulizi yenye lugha ya mjazo(nathari) na mtiririko wake huwa sahihi na rahisi, mara nyingi masimulizi huwa mafupi.
Kuna sifa zinatambulisha utambaji wa hadithi jukwaani, sifa hizo tunaposoma hatuwezi kupata kitabuni, sifa hizo ni  Sauti ya utambaji ambayo husikika moja kwa moja na utambaji wa matukio kwenye jukwaa.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA HADITHI

Kujua muundo wa hadithi –Hadithi huwa ina sehemu tatu Mwanzo, Kati na Mwisho
 1. Mwanzo

Mwanzo wa hadithi hupaswa kuwaandaa wasikilizaji ili waweze kuwa tayari kusikia kile kinachotaka kusimuliwa.
Kwa mfano
Msimuliaji: Hadithi hadithi!
Wasikilizaji: Hadithi njoo uwongo njoo utamu kolea
Msimuliaji: Hapo zamani za kale
Wasikilizaji: Enheeeee(Wakiitikia)
 1. Kati

Hadithi zote huelezwa kwa kifupi na kufuata mambo muhimu kwa maelezo ya moja kwa moja
Kwa mfano: Kuzaliwa….kukua…..kuoa.
 1. Mwisho

Katika sehemu hii ya hadithi mara nyingi huonyesha mwisho wa kisa, kwa mfano kufa, kufanikiwa au kuharibikiwa. Mara nyingi huhitimishwa na maneno kama vile…….Na hadithi yangu ikaishia hapo.

Kisa kinachosimuliwa kinapaswa kuendana na maisha ya jamii husika

Kisa kinachosimuliwa kinapaswa kuendana na wakati.

Msimuliaji wa hadithi anapaswa kutumia lugha fasaha na matamshi sahihi ili wasikilizaji wapate kuelewa.

Mtumiaji atumie wahusika wanaoeleweka kwa wasikilizaji wake, Kwa mfano wahusika wanaweza kuwa wanyama kama vile sungura, fisi au twiga, Pia wanyama wanapaswa kupewa uhusika kulingana na matendo yao, kwa mfano sungura anawakilisha ujanja, simba anawakilisha ubabe na pundamilia anawakilisha uzuri

Msimuliaji anapaswa kutumia lugha ya picha ili aweze kuwavutia wasikilizaji wake, Kwa mfano; Simba alimtazama sungura kwa dharau…. Swala alikuwa anatembea kwa maringo…..simba aliponguruma ardhi yote ilitetemeka

Msimulizi pia anapaswa kutumia vitendo vya maigizo ili kuongeza uhai na msisimko katika hadithi inayosimuliwa, kwa mfano;sehemu ya hasira msimuliaji anapaswa kukunja sura ili kuonyesha hasira.

Msimuliaji pia anapaswa kupangilia matukio katika mtiririko unaofaa kuanzia mwanzo, kati na mwisho 

SIFA ZA HADITHI SIMULIZI
 1. Huhifadhiwa kwa kichwa na kutolewa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya masimulizi
 2. Hadithi simulizi mara nyingi hutumia wakati uliopita. Kwa mfano Hapo zamani za kale au zama zile za mabibi na mababu
 3. Hadithi simulizi huwa fupi na zenye kueleweka.
 4. Hadithi simulizi hutumia wahusika kama vile wanyama pia huweza kutumia wanadamu.

 
DHIMA ZA HADITHI SIMULIZI
Huelimisha jamii, Husaidia jamii kuelewa mambo mbalimbali yaliyopo katika jamii yao
Kujenga jamii kwa kutoa maelezo m,balimbali kutoka kwenye hadithi
Hadithi husistiza ushirikiano katika jamii
Hadithi hurithisha busara toka kizazi kimoja kwenda kingine
Hadithi huburudisha jamii. 
 
USIMULIZI WA HABARI
Ni maneno yanayotolewa na mtu au kundi la watu kuhusu jambo Fulani lililotokea au litakalotokea. Mara nyingi msimulizi wa habari huwa ni yule aliyeona tukio kwa mara ya kwanza au kusikia tukio likisimuliwa toka kwa mtu aliyeona kwa mara ya kwanza.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA USIMULIZI WA HABARI
Kutumia sauti inayosikika; sauti hutumiwa ili msikilizaji aweze kusikia na kuelewa vizuri kile kilichokusudiwa, Pia sauti huweka msistizo pale panapostahiki na kupambanua kauli.

Mpangilio mzuri wa mawazo; Huwezesha wasikilizaji kuelewa mtiririko wa habari au mawazo yanayotolewa

Kutumia lugha fasaha, msimuliaji anapaswa kumjua vizuri msikilizaji wake, wakati anaosimulia na mahali ili aweze kutumia maneno sahihi kulingana na wasikilizaji wake

Ni vizuri habari ikawa fupi ili isiwachoshe wasikilizaji.

Ni vizuri msimulizi kuwa na uhakika way ale anayoyasimulia, kwa kawaida kila habari huwa na ushahidi wa yale yanayosimuliwa.

 

 

 
(This post was last modified: 10-20-2017 01:05 PM by MyElimu.)
10-19-2017 07:00 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 
User(s) browsing this thread: 1 Guest(s)