Uhifadhi Wa Kazi Za Fasihi Simulizi
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
 • 0 Votes - 0 Average
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4
 • 5
Uhifadhi Wa Kazi Za Fasihi Simulizi
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 116 in 77 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,933.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Uhifadhi Wa Kazi Za Fasihi Simulizi

0
0
UHIFADHI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Fasihi simulizi ni aina  fasini ambayo huwasilishwa kwa njia yam domo na vitendo na hupokewa kwa kusikilizwa. Fasihi simulizi imegawanyika katika tanzu nne tofauti ambazo ni;
 1. Maigizo
 2. Semi
 3. Ushairi
 4. Hadithi

 
Kila utenzi wa fasihi simulizi una umuhimu wake, kwa pamoja tanzu zote zina umuhimu wake kwa jamii.
 
Umuhimu wa Fasihi simulizi
 • Hutumika kuelimisha watu, kupitia fasihi simulizi watu hupata maarifa ya kutambua mambo maovu na namna ya kuyakwepa, jamii hujifunza kujitawala, kuzalisha mali na usawa wa demokrasia kupitia kazi za fasihi simulizi.
 • Hutumika kutoa mafunzo kuhusu mambo mbalimbali ya historia, dini, siasa, giografia, uchumi na sheria.
 • Huwapa watu uwezo wa kuzungumza kwa ufasaha, kuigiza mambo kwa ustadi na kucheza ngoma kwa umaridadi.
 • Huhifadhi na kurithisha mambo mbalimbali kuhusu utamaduni kutoka kizazi kimoja kwenda kingine mambo yanayohusu mila na destuli za jamii zao.
 • Hutumika kuburudisha na kuleta msisimko wa kimwili na kiakili
 • Hudumisha na kukuza lugha, watu hupata misamiati mingi zaidi na miundo ya lugha kupitia kazi za fasihi simulizi
 
Njia zinazotumika Katika Kukuza Fasihi Simulizi
 • Kupitia vikundi mbalimbali vya Sanaa na muziki, vikundi hivi vimeanzishwa ili kuendeleza tanzu mbalimbali za fasihi simulizi mfano wa vikundi hivyo ni vikundi vya Sanaa za maonyesho, vikundi vya taarabu na muziki.
 • Wizara ya Elimu kutoa tamko kuwa fasihi simulizi ifundishwe mashuleni kuanzia ngazi ya awali mpaka elimu ya juu.
 • Kupitia wizara ya elimu pia imeanzisha vyuo vya Sanaa za maonyesho kwa mfano chuo cha Sanaa cha Bagamoyo, Butimba, Nyegezi, na vingine.
 • Vyombo vya habari, hivi navyo vinasaidia kukuza na kueneza fasihi simulizi kupitia vipindi mbalimbali vinavyotangazwa kupitia redio, runinga na kwenye magazeti na majarida, kwa mfano Kuna michezo ya kuigiza
 • Kutumia fasihi simulizi kwenye sherehe mbalimbali, kwa mfano kwenye misiba, harusi na mikutano ya siasa hii pia huendeleza na kukuza fasihi simulizi.
 
NJIA ZA UHIFADHI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
 1. Kichwani

Hii ni njia ya mwanzoni kabisa ambayo ilikuwa ikitumika kuhifadhi kazi za fasihi simulizi, tangu zamani imekuwa ikitumika na imeendelea kutumika hata hivi leo. Kwa njia hii, fasihi simulizi huhifadhiwa kichwani na hutumika pale mtu anapohadithia au anaposimulia kwa watu wengine.
 
Ubora wake
 • Uwasilishwaji wake unaweza kufanyika wakati wowote bila kuhitaji maandalizi yoyote ya kabla.
 • Uhifadhi wake hautumii gharama yoyote.
 • Uwasilishwaji wake ni hai, hii ni kwa sababu msimulizi huwa yuko ana kwa ana na hadhira yake kwahiyo anaweza kubadilisha sauti, au miondoko ili kuelezea hisia tofauti tofauti.
 
Udhaifu wake
 • Kuna uwezekano mkubwa wa kazi ya fasihi kupotea pale ambapo msanii wa kazi ya fasihi atapata ugonjwa wa kusahau, au kufariki kazi iliyohifadhiwa kichwani hupotea.
 • Ni rahisi kubadilika na kupoteza uhalisia wake wa awali, hii ni kwa sababu msanii anaweza kupoteza baadhi ya matukio ya fasihi kwa kusahau au kuamua kubadilisha ujumbe uliopo.
 
 
 1. Njia ya maandishi

Njia hii imeanza kutumika baada ya watu kujua kusoma na kuandika. Uhifadhi wa kazi za fasihi kwa njia hii hupitia katika hatua mbili mojawapo ni kwa kubuni kisa au wazo na hatua ya pili ni kuliweka wazo hilo katika maandishi.
Ubora wake
 • Kazi huhifadhiwa katika hali inayoweza kudumu katika kipindi kirefu
 • Huweza kufikia hadhira iliyo mbali toka mahali alipo msanii.
 • Kupitia njia hii ya kuhifadhi kazi ya fasihi haiwezi kupotea.
Udhaifu wake
 • Njia hii hutumiwa na wale wanaojua kusoma tu.
 • Hadhira yake ni ya wale wanaojua kusoma tu.
 • Wahusika yaani msanii na hadhira yake hawaonani.
 • Huhitaji gharama katika kuhifadhi kazi ya fasihi, maandalizi yake huhitaji vitu kama vile peni, karatasi, meza na kiti, vitu hivyo vyote huhitaji fedha ili kuvinunua.
 • Hupunguza uhalisia kwa sababu msanii hawezi kutumia matendo katika usimulizi ulio katika njia ya maandishi.
 
 1. Njia ya Vinasa sauti

Hii ni miongoni mwa njia zinazotumika kuhifadhi kazi ya fasihi simulizi, njia hii ni endelevu zaidi kulinganisha na njia ya maandishi na njia ya kichwa. Njia hii imeanza kutumika baada ya uvumbuzi wa vyombo vya vya kisayansi hasa redio ambayo hurekodi sauti tu.
Ubora wake.
 • Kazi ya msanii huweza kuwafikia hata hadhira iliyo mbali na mahali alipo msanii au mtunzi wa kazi ya fasihi.
 • Kazi ya fasihi huwa haiwezi kupotea wala kuharibika ikiwa itahifadhiwa vizuri.
 • Hutunza kumbukumbu kwa muda mrefu
 
 
Udhaifu wake
 • Hutumia gharama kubwa ili kuweza kurekodi kazi ya fasihi, hii ni kwasababu huhitaji kununua vinasa sauti ambavyo huuzwa kwa bei kubwa.
 • Uwasilishwaji wake sio hai hii ni kwasababu wahusika hawaonani wanasikia kwa sauti tu.
 • Kazi ya fasihi hubaki mali ya msanii aliyerekodi, mtu mwingine hana ruhusa ya kutumia kazi hiyo bila ruhusa.
 • Haiwezi kubadilishwa pale inaporekodiwa hata kama itapitwa na wakati na mazingira yakawa tofauti.
 
 1. Njia ya kompyuta

Njia hii imeanza kutumika katika miaka ya hivi karibuni baada ya watu wengi kuanza kuelewa namna ya kutumia kompyuta.
Ubora wake
 • Njia hii ni ya uhakika zaidi, kazi zote huhifadhiwa katika komputa na hutolewa pale zinapohitajika.
 • Haiwezi kupotea kwa urahisi
 
Udhaifu wake
 • Msanii na hadhira hawawasiliani ana kwa ana, kazi ya fasihi inapunguza uhai wake.
 • Hadhira hukosa nafasi ya kuuliza maswali kwa vipengele ambavyo vina utatanishi.
 • Lazima msanii awe anajua namna ya kutumia kompyuta.
 • Njia hii ni ya gharama kubwa zaidi kulinganisha na njia nyingine.
 
 
 
 
 1. Njia ya kanda za video

Njia hii hurekodi sauti, sura na  matendo ya msanii ambayo yanafanyika katika kuwasilisha kazi ya fasihi simulizi.
 
Ubora wake
 • Wasanii na vifaa vinavyotumika huonekana, hivyo huongeza uhai katika kazi ya fasihi.
 • Ni njia ya uhakika zaidi na hudumu kwa muda mrefu kama kanda zilizotumika zitahifadhiwa vizuri.
 
Udhaifu wake
 • Njia hii ina gharama kubwa, msanii hutakiwa kununua vifaa kama vile runinga, kanda tupu na kumlipia mpiga picha na atakayerekodi kazi ya fasihi.
 • Huwafikia wachache, hufika kwa wale wenye uelewa na uwezo wa kuwa na vifaa kama runinga wengine hawawezi kufikiwa na kazi hizi.
 • Hakuna mawasiliano ya ana kwa ana kati ya msanii na hadhira.
 
 1. Njia ya makazi

Njia hii hutumika kuhifadhi zaidi ala za kisanaa kama vile ngoma, marimba, zeze, na mazao tofauti ya Sanaa na ufundi kama vile vinyago, mikeka, na picha za kuchora. Kwa kutumia njia hii msanii huzikusanya kazi zake na kuzuhifadhi nyumbani kwake.
Ubora wake
 • Kazi zinapohifadhiwa katika nyumba huweza kubaki salama kwa muda mrefu.
 • Msanii hutumia gharama ndogo kuonyesha Sanaa yake kwasababu ya umiliki wa vifaa vya kazi yake.
 
 
Udhaifu wake
 • Ni rahisi kuharibika kama vyombo vya kazi za fasihi vitahifadhiwa vibaya.
 • Ni rahisi vyombo vya kazi ya fasihi kuibiwa kama hakuna ulinzi wa kutosha.
 • Ajali kama ya moto na mafuriko huwezi kuteketeza kazi ya Sanaa hiyo.
 
 
Umuhimu wa Kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi
 • Husaidia kukuza na kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali.
 • Fasihi simulizi ni sehemu ya ajira pia kama itatumika kwa lengo la kuingiza fedha.
 • Kazi za fasihi simulizi pia huweza kutumika kama vivutio vya utalii
 • Huingizia pato taifa kama kutakuwa na njia tofauti za kuhakikisha kazi za fasihi zinatumika ili kuongeza kipato.
 
            
 
12-04-2017 02:32 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Simulizi MyElimu 0 2,007 12-04-2017 02:27 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon Fasihi Kwa Ujumla MyElimu 0 3,775 09-14-2017 01:19 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon Nyimbo Katika Fasihi Simulizi MwlMaeda 0 1,314 06-09-2017 12:23 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Udhibiti Wa Kazi Za Fasihi Kwa Ufupi MwlMaeda 0 1,105 06-08-2017 07:09 PM
Last Post: MwlMaeda
  Madoido Katika Fasihi MwlMaeda 0 633 06-07-2017 10:57 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Mofimu Na Kazi Za Mofimu MyElimu 0 4,708 05-15-2016 12:10 AM
Last Post: MyElimu
Lightbulb Tanzu na Vipera Vya Fasihi Simulizi Given 1 32,384 12-21-2015 11:07 AM
Last Post: SUSAN MACHARIA
Post Icon Fani Na Maudhui Katika Fasihi MyElimu 0 10,325 09-12-2014 02:17 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon Siti Binti Saadi - Mtunzi mkongwe wa Fasihi ya Kiswahili Given 0 2,386 02-20-2014 11:40 PM
Last Post: GivenUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)