Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Simulizi
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
 • 0 Votes - 0 Average
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4
 • 5
Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Simulizi
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 116 in 77 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,933.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Simulizi

0
0
UHAKIKI WA KAZI FASIHI SIMULIZI
FASIHI SIMULIZI
Uhakiki ni kitendo cha kusoma kazi ya fasihi simulizi na kuchambua vipengele vya fani na maudhui kwa kuangalia ubora na udhaifu wa kazi hiyo.
Mhakiki ni yule mtu anayechambua kazi ya fasihi simulizi na kuchunguza vipengele vya fani na maudhui.
Kazi ya Uhakiki
 • Kuelewesha hadhira kuhusu kuwepo na kazi hiyo.
 • Kuchambua vipengele vya fani na maudhui.
 • Kueleza ubora na upungufu wa kazi hiyo
 • Kueleza umuhimu wa kazi hiyo
                                                     
VIPENGELE VINAVYOFANYIWA UHAKIKI
 1. Fani
 • Wahusika
 • Mtindo
 • Muundo
 • Mandhari
 • Matumizi ya lugha.
 
 1. Maudhui
 • Dhamira
 • Falsafa
 • Mtazamo/ Msimamo
 • Ujumbe
 • Migogoro
 
Kazzi za fasihi simulizi zinazofanayiwa uhakiki ni kama vile mashairi, maigizo na hadithi.
 
UHAKIKI WA MASHAIRI
Mashairi ni kazi ya fasihi simulizi ambayo mhakiki huchunguza vipengele vya fani na maudhui. Katika fani mhakiki huchunguza ufundi alioutumia mtunzi katika kutunga kazi yake na katika maudhui mtunzi huchunguza mawazo muhimu yaliyojitokeza katika kazi hiyo.
 • Mtindo
Hapa mhakiki anaangalia shairi kama ni la kimapokeo au la kisasa. Mashairi ya kimapokeo ni mashairi yanayofuata …….
 
 • Muundo
Ni kipengele ambacho msanii huweka wazi mambo kama vile idadi ya beti katika shairi, idadi ya mistari na aina za vibwagizo.
Kwa mfano;
 1. Mistari 4- Tarbia
 2. Mistari 2 – Tathnia
 3. Mistari 3 – Tahlitha
 4. Mstari 1 – Tamalitha

 
Mfano;
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli, iwafae maishani,
Muundo wa Tarbia
 
 • Wahusika
Katika mashairi kunakuwa na wahusika ambao wanaweza kuwa viumbe hai au wasio hai.
 • Matumizi ya lugha
Hapa mhakiki lazima achunguze vitu vifuatavyo;
Mpangilio wa maneno, Kwa mfano mweupe paka badala yap aka mweupe
Ufupisho wa maneno kwa mfano wembe badala ya kiwembe
Matumizi ya methali, misemo na nahau
Matumizi ya picha
 
 
12-04-2017 02:27 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Uhifadhi Wa Kazi Za Fasihi Simulizi MyElimu 0 3,682 12-04-2017 02:32 PM
Last Post: MyElimu
  Uhakiki MOH'D SALIM MOH'D 0 1,192 09-17-2017 12:06 PM
Last Post: MOH'D SALIM MOH'D
Post Icon Fasihi Kwa Ujumla MyElimu 0 3,775 09-14-2017 01:19 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon Nyimbo Katika Fasihi Simulizi MwlMaeda 0 1,314 06-09-2017 12:23 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Udhibiti Wa Kazi Za Fasihi Kwa Ufupi MwlMaeda 0 1,105 06-08-2017 07:09 PM
Last Post: MwlMaeda
  Madoido Katika Fasihi MwlMaeda 0 633 06-07-2017 10:57 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Mofimu Na Kazi Za Mofimu MyElimu 0 4,708 05-15-2016 12:10 AM
Last Post: MyElimu
Lightbulb Tanzu na Vipera Vya Fasihi Simulizi Given 1 32,384 12-21-2015 11:07 AM
Last Post: SUSAN MACHARIA
Post Icon Uhakiki Wa Tamthiliya Ya Kilio Chetu MyElimu 0 18,135 03-02-2015 10:50 AM
Last Post: MyElimu
Post Icon Fani Na Maudhui Katika Fasihi MyElimu 0 10,325 09-12-2014 02:17 PM
Last Post: MyElimuUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)