Uchambuzi Wa Wasakatonge
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Uchambuzi Wa Wasakatonge
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 110 in 72 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,929.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Uchambuzi Wa Wasakatonge

0
0
Diwani ya Wasakatonge ni miongoni mwa diwani zilizochapishwa mwanzoni mwa karne ya ishirini na moja zikionesha changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii yetu. Mwandishi wake ni mtunzi mahiri Mohammed S Khatibu.

MAUDHUI

Maudhui hujumuisha dhamira, ujumbe, migogoro, falsafa, mtazamo au msimamo wa mwandishi.
UMASKINI
Mwandishi ameonyesha kuwa jamii imegubikwa na wimbi la umaskini. Katika shairi la “Wasaka Tonge”, msanii anasema watu wanashindwa kupata mahitaji muhimu na ya lazima ya kila siku. Mfano wa watu hawa ni wabeba zege, yaya na wengineo. Anasema:
[Image: SuperStock_1850-18460.jpg]
“jua kali na wasakatonge
Wao ni manamba mashambani,
Ni wachapakazi viwandani,
Mayaya na madobi wa nyumbani,
Ni matopasi wa majaani,
Lakini bado ni maskini”
MARADHI
Katika shairi la “Tina Isotibu” Tunaambiwa kuwa mbali na Bara la Afrika kuwa na tatizo la janga la umaskini, pia limeendelea kukumbwa na tatizo la maradhi. Msanii anasema,
[Image: against-malaria.jpg]
“Lakini
Vidonge chungu ajabu,
Dawa zake hazitibu
Zimeizidisha tabu
Mgonjwa kumwadhibu
haipo tiba”
 
 
 
UONGOZI MBAYA (UDIKTETA)
Diwani hii imebainsha saratani ya udikteta unaoikabili dunia ya leo. Udikteta umeota mizizi katika dunia hii kiasi cha kuwafanya watu waishi kwa hofu. Katika shairi la madikteta msanii anasema,
[Image: idi.jpg]
“Itele “Mungu watu”
Bokasa, Idi, Mobutu.
mizinga nayo mitutu
Haitoi risasi
Hutoa maraisi
Walio madikteta
 
 
MAPENZI
Hii ni moja ya dhamira ambazo zimeonyeshwa na mwandishi kwa kina. Msanii anaonyesha kuwa mapenzi kati ya watu na mtu ni faraja amani na utulivu na ni kiungo kati ya mume na mke. Katika shairi la “Mahaba” msanii anasema,
[Image: IMG_18229607514502.jpeg]
“Kama mahaba wazimu, sihitaji nitibiwe
Bora niwe chakaramu, nipigae watu mawe
Kuwa kwangu mahamumu, wewe usi kusumbuwe
Dawa yangu si ngumu, mimi nipendwe na wewe
Mshairi mengine ambayo yanazungumzia mapenzi ya dhati ni pamoja na “Nilikesha”
Na “Sili Nikashiba’ .
 
 
 
 
Vilevile msanii amezungumzia mapenzi ya ulaghai katika shairi la “Si Wewe”. Msanii anaonyesha ni kwa jinsi gani mapenzi ya ulaghai yanaweza kusababisha majeraha, hasira na majuto miongoni mwa wawili hao. Msanii anasema,
“Umeshapwelewa nchi kavu,
Wako werevu umekwisha,
Sasa unatweta
U taabani
Ni wewe ulo mlafi”
Si wewe?
UNAFIKIMsanii amekemea suala la unafiki katika jamii zetu, mwandishi anaonyesha kuwa wapo waumini na viongozi wa dini ambao wamekuwa wakijigamba mbele za watu kuwa wako safi wakati matendo yao ni kinyume na waonavyosema, Katika shairi la ‘WASO DHAMBI, mwandishi anasema,
Misalaba, na majuba, na hotuba,
Nyingi toba, zenye hiba, na haiba,
Mambo yao,
Unafiki”
(This post was last modified: 11-05-2014 10:59 AM by MyElimu.)
11-05-2014 10:49 AM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Gift Armstrong Offline
Regular User
Registered

Posts: 1
Likes Given: 0
Likes Received: 0 in 0 posts
Joined: Aug 2015
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 0.00 points
Post: #2
RE: Uchambuzi Wa Wasakatonge

0
0
Nimependa uchambuzi wa diwani ya wasakatonge na penda kujua na kitabu cha chekacheka pamoja na maswali yake(any one can help me)
08-12-2015 01:15 AM
Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Emmanuel Alphonce Msabila Offline
Regular User
Registered

Posts: 3
Likes Given: 2
Likes Received: 0 in 0 posts
Joined: Jan 2016
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 0.00 points
Post: #3
RE: Uchambuzi Wa Wasakatonge

0
0
Nimependezewa Na Uchambuzi Wako.
01-30-2016 03:48 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
Post Icon Uchambuzi Wa 'watoto Wa Mama Ntiliye' MyElimu 1 1,192 08-18-2017 11:54 AM
Last Post: riddah chory
Post Icon Uchambuzi Wa Takadini MyElimu 0 1,203 10-31-2016 11:19 AM
Last Post: MyElimu
Post Icon Uchambuzi wa Riwaya ya MFADHILI MyElimu 1 6,444 12-18-2015 02:19 PM
Last Post: neema rajab
Post Icon Uhakiki Wa Diwani Ya Wasakatonge MyElimu 0 30,541 09-12-2014 02:06 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon UCHAMBUZI: Diwani ya FUNGATE YA UHURU MyElimu 0 6,451 02-24-2014 12:59 AM
Last Post: MyElimuUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)