Uandishi Wa Insha
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Uandishi Wa Insha
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 111 in 73 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,931.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Uandishi Wa Insha

0
0
UANDISHI WA INSHA
Insha ni mfululizo au mfuatano wa sentensi zenye mtiririko zinazoeleza kuhusu mada Fulani. Mawazo katika insha hupangwa katika aya na kila aya hubeba wazo lake.
MUUNDO WA INSHA
Kichwa cha insha,
Kichwa cha Insha huandikwa juu kabisa ya karatasi kwa herufi kubwa na hupigwa mstari na kisizidi maneno matano.
Mfano; ATHARI ZA UKIMWI                                                                                               UMUHIMU WA KUTUNZA MAZINGIRA
  •  
hueleza kwa ufupi juu ya jambo ambalo insha inazungumzia, ni sehemu muhimu sana kwani huvuta hisia za msomaji kuendelea kusoma insha iliyoandikwa. Utangulizi unatakiwa kuwa na aya moja tu.
Kiini cha insha,
Kiini cha insha ndio insha yenyewe hapa mwandishi hueleza kwa undani jambo au mada anayozungumzia.
Mwisho wa insha,
Mwisho wa insha ni maelezo mafupi yanayoelezea yale insha iliyokuwa inayaelezea, inaweza kuwa ni kutoa maoni,ushauri na mapendekezo ya nini kifanyike.
 
 
 
AINA ZA INSHA
Insha za kisanaa
Ni aina ya insha ambayo huandikwa kwa kuzingatia lugha ya kifasihi lugha yenye misemo,nahau,methari na tamathali za semi.
Sifa za insha za kisanaa
Ili ziitwe insha za kisanaa ni lazima ziwe na vitu vifuatavyo
Utenzi wa maneno yaani maneno yenye mvuto
Lugha ya kisanaa(Lugha ya kifasihi)
 
Insha zisizo za kisanaa
Ni zile insha ambazo hazitumii lugha ya kifasihi. Mfano wa insha zisizo za kisanaa ni insha za wasifu.
Insha za wasifu
Ni insha zinazoeleza sifa kuhusu mtu au kitu fulani.
 
Taratibu za uandishi wa insha
Ni lazima ubuni jambo la kuandika
Ni lazima ibebe ujumbe fulani
Ni lazima kuwepo na dhamira au wazo kuu
Ni lazima kuhusisha visa na mkasa
Utenzi wa maneno
Utambue kanuni za uandishi mfano alama za uandishi.
          Alama ya nukta (.)
          Alama ya kiulizo (?)
          Alama ya mkato (,)
Mfano wa insha
                                ATUKUZWE NYERERE WA TANZANIA    
Nyerere wa Tanzania, kiongozi shujaa wa dunia – amepata kutukuka pande zote za dunia. Alizaliwa katika kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara. Alisoma elimu ya msingi katika shule ya Mwisenge – mojawapo ya shule za zamani sana hapa nchini. Alipata elimu ya sekondari huko Tabora. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda kabla ya kwenda huko Uingereza kusomea shahada ya M.A.
Baada ya uhuru toka Uingereza, Mwalimu Nyerere alishughulika sana na suala la ukombozi wa Tanganyika na Afrika kwa ujumla. Alionesha jitihada za wazi kupambana na mabeberu wa Kiingereza hadi uhuru wa Tanganyika ukapatikana tarehe 9/12/1961. Tanganyika ikawa ya kwanza kupata uhuru wake ukilinganisha na cnhi zote za Afrika ya Mashariki na kati  sifa kuu kwa Nyerere wa Tanganyika.
Nyerere alishirikiana na Karume kuziunganisha nchi hizo na kuzaa Tanzania jina lililotumika na kuheshimiwa kote ulimwenguni. Wakati Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar alitamka maneno ya hekima yafuatayo:
 
 “Tumeamua kuziunganisha nchi zetu ili kuimarisha umoja wa Afrika. Naamini kuwa maadui wetu watachukia na kuhuzunika kwa kitendo hiki cha kishujaa tulichokifanya, lakini daima hatutaogopa chochote. Muungano wetu utadumu milele na milele. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika. Amina!”
 
Sifa ya pekee inayomtofautisha Mwalimu Nyerere unapomlinganisha na wanafalsafa wengine duniani kama vile Karl Marx na Mao ni kwamba yeye aliwapigania wanyonge wote kote ulimwenguni bila kujali ubaguzi wa rangi, kabila, taifa au bara. Aliwatetea wanyonge wa Afrika. Aliwapigania wanyonge wa Ulaya na Mashariki. Aliwapigania wanyonge wa bara la Asia. Halii kadhalika aliwapigania na kuwatetea wanyonge wa bara la Amerika ya Kusini. Hivyo ni sifa ya pekee inayofaa kumtofautisha na wanafalsafa wengine waliomtangulia.
Nyerere atatukuzwa daima kwa ushujaa wake. Alikuwa si kiongozi wa kujikombakomba kwa matifa mengine ya kibeberu. Alipotishiwa au kuwekewa vikwazo/vitisho, alivunja mara moja uhusiano wa kidiplomasia na taifa linalohusika. Kwa mfano mwaka 1965 alivunja uhusiano wa kidiplomasia nan chi ya Uingereza baada ya nchi hiyo kuitangaza nchi ya Zimbabwe kama koloni lake la kudumu la Walowezi. Kitendo hiki kilimpatia sifa na heshima kubwa hapa Afrika na duniani kote kwa wapenda amani.
Ingawa ni vigumu kuzitaja sifa zake mpaka mwisho, lakini sifa ya kupiga makelele katika majukwaa ya kimataifa haitaweza kusahaulika. Hakuwa msomi mkimya kama wasomi wa enzi hizi. Alitumia elimu yake ipasavyo kuitetea falsafa yake ya Haki na Usawa kwa Binadamu Wote katika majukwaa ya kimataifa.
Wananchi wa Uganda daima humkumbuka na kumtukuza kwa jinsi alivyotumia nguvu za kijeshi kuung’oa utawala wa kidikteta wa Nduli Idd Amini Dada. Wakikumbuka mateso waliyoyapata enzi za utawala huo, humtukuza na kumuenzi Nyerere usiku na mchana.
Nyerere hataweza kusahaulika kwa jinsi alivyopinga kitendo cha viongozi wachache wenye hila kuendelea kung’ang’ania kwenye madaraka. Alikuwa kiongozi wa kwanza hapa Afrika na pengine duniani kote kung’atuka kwenye kiti cha Urais. Alifanya hivyo kwa hiyari ili kutoa nafasi kwa wananchi wengine washike nyadhifa hii nyeti hapa nchini kwetu.
Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa hekima na busara. Kinywa chake daima kilinena maneno ya hekima na busara. Fikra zake zitadumu milele kwenye vichwa vya wakulima, wasomi, wanafalsafa, mapadri, masheikh, wachungaji, watawa na hata kwenye bongo za waovu wa Tanzania daima watamkumbuka.
Kifo cha Mwalimu Nyerere kimeleta pengo kubwa kwa jamii yote ya wapenda amani kote ulimwenguni. Ingekuwa mbegu yam mea tungeipanda sote tuendelee kuhekimika kutokana na hekima na busara zake.
Kifo cha Mwalimu Nyerere ni kama mwindaji asiye na silaha kwenye mwitu wenye wanyama wakali kama fisi, simba, ngiri, tembo, nyoka, nyati, n.k. Je, mwindaji atafanya nini?
 
Daima sifa na hekima za Mwalimu Nyerere zitukuzwe Tanzania, Afrika na ulimwenguni kote.
                            
          

 
10-19-2017 07:11 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Uandishi MyElimu 0 692 12-04-2017 02:45 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon Uandishi Wa Barua MyElimu 0 1,551 10-19-2017 07:21 PM
Last Post: MyElimu
  Utungaji/uandishi MwlMaeda 0 6,401 07-14-2017 06:42 AM
Last Post: MwlMaedaUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)