Shairi: Nani Katia Shubiri?
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Shairi: Nani Katia Shubiri?
MwlMaeda Offline
Teacher
Teacher

Posts: 41
Likes Given: 1
Likes Received: 3 in 3 posts
Joined: Feb 2017
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 3,446.38 points
Country: Tanzania
Post: #1
Shairi: Nani Katia Shubiri?

0
0
KUTOKA KATIKA KITABU CHA KUMBUKIZI

MTUNZI: MBARUKU ALLY
SHAIRI: NANI KATIA SHUBIRI?

Mwanzo ilikuwa tamu, tena isiyo dosari
Utamu ungalidumu, ila mejaa hatari
Leo nashika kalamu, kumwuliza Daktari
Nani katia shubiri, kwenye tungi la asali?

Asali kwenye mzinga, chungu meingia vipi?
I ndani siwezi pinga, sijui yatoka wapi
Muuliza si mjinga, hata angekuwa yupi
Nani katia shubiri, kwenye tungi la asali?

Imeingia simanzi, vijana kushika tama
Hakuna anomaizi, zina nini hizi zama
Mua kugeuka bunzi, na mfupa kuwa nyama
Nani katia shubiri, kwenye tungi la asali?

Tupigane na adui, ingawa haonekani
Kwa macho hautambui, hujui nini ni nini
Hata kama ni bedui, hukutoa duniani
Nani katika shubiri, kwenye tungi la asali?

Jamani nipeni jibu, yoyote mwenye kujua
Waganga nimejaribu, sina nililoambua
Swali linonipa tabu, ninataka kutambua
Nani katia shubiri, kwenye tungi la asali?

MBARUKU ALLY
MOTO WENU
0717199835
25/09/2011

Ni shairi nililolitunga nikiwa shule ya sekondari Mivumoni Islamic Seminary Dar es salaam mwaka 2011

Karibu: http://www.mwalimuwakiswahili.com
07-16-2017 02:57 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Shairi: Tanga Rudi Masomoni MwlMaeda 1 312 06-08-2017 01:11 PM
Last Post: AchieverUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)