Mofimu Na Kazi Za Mofimu
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Mofimu Na Kazi Za Mofimu
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 110 in 72 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,929.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Mofimu Na Kazi Za Mofimu

0
0
 Mofimu, ni kipashio kidogo kabisa cha kiisimu ambacho kina maana ya kisarufi au ya kileksika (kikamusi)Mofimu ni kipashio kidogo kuliko neno(MOFIMU, NENO, KIRAI, KISHAZI NA SENTENSI)Kutokana na muanisho hapo juu, kipashio kidogo kuliko vyote ni mofimu na kikubwa kuliko vyote ni sentensi

Pia mofimu ni kipashio kidogo kabisa kiltacho maana kamili kisarufi au kileksika (kikamusi)Mfano,
a) Analima;  A-na-lim-a (neno analima lina mofimu nne)            
b) Mtoto; M-toto ( neno mtoto lina mofimu mbili)

AINA ZA MOFIMU
Kuna aina mbili za mofimu, aina izo ni
a)      Mofimu huru
b)      Mofimu tegemezi

A: MOFIMU HURU
Hii ni aina ya mofimu inayoweza kusimama peke yake na kuleta maana bila kua na kiambishi chochote. Mofimu huru zina hadhi ya neno na zinaweza kuwa aina yoyote ya neno kama vile;NOMINO- Juma,mama,babuVITENZI- Sali, sameheVIVUMISHI-safi,chafu,bidii 

B: MOFIMU TEGEMEZI
Mofimu tegemezi, hizi ni aina za mofimu zinazofungamana na mofimu zingine ili kutoa maana iliyokusudiwa na zinapotumika hutegemea ili kueleza dhana iliyokusudiwa. Mofimu hizi zinakua mbili au zaaidi kulingana na mchangamano wa dhana ulio katika neno linaloundwa.Mfano;Neno- Analima- (A-na-lim-a) lina mofimu nne.Mofimu tegemezi ni (A,na,a) na zina dhima tofauti tofauti. Mofimu tegemezi zimeitwa hivyo kwa sababu haziwezi kusimama peke yake na kuleta maana.Mofimu tegemezi hupachikwa katika mzizi (kiini) ni ile sehemu ya neno ambayo hubeba maana ya msingi ya neno na haibadiliki.

 
05-15-2016 12:10 AM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Uhifadhi Wa Kazi Za Fasihi Simulizi MyElimu 0 998 12-04-2017 02:32 PM
Last Post: MyElimu
  Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Simulizi MyElimu 0 569 12-04-2017 02:27 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon Udhibiti Wa Kazi Za Fasihi Kwa Ufupi MwlMaeda 0 695 06-08-2017 07:09 PM
Last Post: MwlMaedaUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)