Kisa: Kuku Kitoweo Murua Kwa Walaji!!!
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Kisa: Kuku Kitoweo Murua Kwa Walaji!!!
MwlMaeda Offline
Teacher
Teacher

Posts: 41
Likes Given: 1
Likes Received: 3 in 3 posts
Joined: Feb 2017
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 3,446.38 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Kisa: Kuku Kitoweo Murua Kwa Walaji!!!

0
0
KUKU KITOWEO MURUA KWA WALAJI!!!

Ukipita sokoni ukawakuta kuku wakiwa kwenye *tenga* jaribu kuwatizama mara mbili mbili kisha jiulize maswali kibao!.
Ulipowatizama umewaona wakiwa na huzuni au furaha?.
✍Kwa utafiti niliofanya katika masoko mengi nimewakuta kuku wakiwa _wamechangamka sana!, na hasa kama wakiwa wamewekewa chakula wanachokipenda sana!
✍Kuku wengine _hufikia hatua ya kugombana kutokana na chakula walichowekewa katika tenga lile!!
✍Wakati mwingine nimewahi kushuhudia _majogoo yenye nguvu yakionesha ubavu kwa majogoo dhaifu na pengine hata kuyatia kashikashi yasile chochote kilicholetwa pale tengani!
✍Jambo jingine kubwa nilio liona _ni majogoo yenye nguvu kujimilikisha majike yote yalioko kwenye tenga lile!, huku majogoo dhaifu yakiumia kwa kukosa haki yao ya kimsingi!
?Hayo ni mambo makubwa manne ambayo mimi na wewe tumewahi kuyaona mubashara kwa kuku wa tengani!, lakini _*je, tumewahi kujiuliza maswali na kupata ibra ya matukio hayo?
*Ibra ya kwanza!*: Hawa _kuku wote walioko tengani, bila kujali jogoo wala jike, wooote maadamu wako tengani hawako huru_. Wakilifahamu hilo ni hatua nzuri!
*Ibra ya Pili!* : Yale majogoo yenye nguvu yanapaswa kuelewa kwamba _hata yenyewe hayako salama bali ni kitoweo murua kinachosubiri wanunuzi tu!!!_. Yakifahamu hili ni hatua nzuri!
*Ibra ya tatu!*: Yale majogoo yenye nguvu _yatumie nguvu yalizonazo sio kuwapiga kuku wenzao bali kujinasua na kuwanasua wengine kutoka kwenye tenga ili yasiwe kitoweo!!!_ Yakifahamu hili ni hatua nzuri!
*Ibra ya nne!*: Kuku wote wanapaswa kufahamu kwamba _huduma nzuri wanazofanyiwa wakiwa kwenye tenga si ishara ya huruma na mapenzi ya dhati dhidi yao_. Hilo wakilifahamu ni hatua nzuri!.
*Ibra ya tano!:*. Wale kuku dhaifu wanapaswa kuelewa kwamba _uhuru sahihi waliokosa hautokani na yale majogoo yanayojifaragua kwenye tenga!!!_. Wakilifahamu hili ni hatua nzuri!
06-10-2017 12:33 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Kisa Cha Nge Na Mzee MwlMaeda 0 553 06-09-2017 10:51 AM
Last Post: MwlMaedaUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)