Kisa Cha Nge Na Mzee
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Kisa Cha Nge Na Mzee
MwlMaeda Offline
Teacher
Teacher

Posts: 41
Likes Given: 1
Likes Received: 3 in 3 posts
Joined: Feb 2017
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 3,446.38 points
Country: Tanzania
Post: #1
Kisa Cha Nge Na Mzee

0
0
KISA CHA NGE NA MZEE.

MZEE mmoja aliona nge akitapatapa kuzama kwenye maji. Imani na roho ya kusaidia ikamjia, akaingiza mkono majini ili kumhami. Alipomgusa tu, nge akamgonga. Maumivu aliyoyapata, alijikuta akitoa mkono bila kumuokoa.

Pamoja na maumivu ya sumu ya nge, mzee alipotupa macho tena majini, alimwona nge akizama na kutapa. Haraka aliingiza mkono ili kumsaidia. Na kama awali, nge akamgonga tena na kumwachia maumivu makali.

Kijana aliyekuwa amesimama kando, alimuuliza mzee: "Kumradhi mzee, naona kama utadhurika bure. Hivi huoni kila unapojaribu kumsaidia, naye anazidi kukugonga?"

Mzee alijibu, "Uhalisia wa nge ni kugonga, uhalisia wangu kama mwanaadamu ni kusaidia. Uhalisia wangu wa kusaidia, hauwezi kubadilika kama ambavyo uhalisia wa nge wa kugonga usivyobadilika."

Punde, mzee alichukua kipande cha mti, akakitumia kumuopoa yule nge na kumtoa nje ya maji. Kijana akaandoka kichwa chini, mikono nyuma.

FUNZO: Kamwe usijibadili uhalisia wako. Ukifanya ihsani ukalipwa nuksani, usibadilike. Badala yake, chukua tahadhari kisha badili mfumo wako wa kusaidia. Hutokea kipindi mtu akakudhuru si kwa makusudi, bali kwa mapungufu yake ya kimaumbile. Kwahivyo, kulipizia uovu ni kujidhulumu nafsi na kujishushia hadhi na heshima yako........


nadhan umejifunza jambo........

Karibu: http://www.mwalimuwakiswahili.com
06-09-2017 10:51 AM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
Post Icon Kisa: Kuku Kitoweo Murua Kwa Walaji!!! MwlMaeda 0 413 06-10-2017 12:33 PM
Last Post: MwlMaedaUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)