Aina Za Maneno
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
 • 0 Votes - 0 Average
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4
 • 5
Aina Za Maneno
MyElimu Offline
System
*******

Posts: 247
Likes Given: 7
Likes Received: 111 in 73 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 1
Friend:  Add as Friend

Points: 3,931.20 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Aina Za Maneno

0
0
Neno ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazobeba maana. Maneno yanaopangwa kwa utaratibu maalumu huunda sentensi, Kuna aina tofauti za maneno ambazo ni
Nomino
Viwakilishi
Vivumishi
Vitenzi
Vielezi
Viunganishi
Vihisishi
 1. Nomino

Nomino ni neno au maneno yanayotaja majina yya watu, vitu, hali, na mahali katika sentensi. Nomino huwekwa mahali penye nafasi ya mtendaji, mtendwa au mtendewa.
Nomino huwa katika hali ya Umoja au wingi
Kwa mfano;
Umoja
 1. John amefaulu mtihani.
 2. Shule imejengwa kijijini
 3. Mwalimu anafundisha vizuri

Wingi
 1. Wanafunzi wanacheza darasani
 2. Magari yanayobeba wanafunzi yamegongana
 3. Vitabu vyote vimepotea.

Aina za Nomino
Kuna aina 4 za Nomino
(a) Nomino za Pekee
(b) Nomino za Kawaida
© Nomino za Jamii
(d) Nomino za Dhahania

(a) Nomino za Pekee
Nomino za pekee hutaja majina maalumu ya vitu au watu wenye maumbile au sifa za kipekee. Nomino zote zilizopo kwenye aina hii huandikwa kwa herufi kubwa kwenye sentensi hata kama Nomino hiyo haitokuwa mwanzo wa sentensi.
Kwa mfano
*majina ya watu binafsi kama vile Julius, Mwajuma, Kagame, na Paulo
*Majina ya Siku kama vile Jumatatu, Jumanne, Alhamisi na Jumapili
*Majina ya milima kama vile Mlima Kilimanjaro, Mlima Meru na Milima ya Uruguru.
 
 (b) Nomino za Kawaida
Ni aina za nomino ambazo hutaja maijna ya jumla ya vitu venye umbile moja kwa mfano Watu, Mimea na wanyama. Aina hii ya nomino huandikwa kwa herufi ndogo isipokuwa kama itatumika mwanzo wa sentensi.
Kwa mfano: mvulana, msichana, ng’ombe, mbuzi.

© Nomino za Jamii
Ni aina za Nomino ambazo hutaja majina ya watu au vitu katika makundi, Aina hii ya Nomino pia huandikwa kwa herufi ndogo isipokuwa kama zitatumika mwanzo wa sentensi.
Mfano wa Nomino hizo ni kikosi, darasa, wanafunzi, wafanyakazi, walimu.

(d) Nomino Dhahania
Ni aina ya Nomino ambayo hutaja vitu, tabia, matukio au matendo ambayo ni ya kufikirika tu. Aina hii ya nomino huhusisha majina ya hali, dhana au mambo ambayo watu hujenga picha zake akilini.
Nomino hizi pia Huandikwa kwa herufi ndogo isipokuwa kama zitatumika mwanzo wa sentensi Kwa Mfano Huzuni, Upendo, Umasikini, Shetani.

2. VIWAKILISHI
Ni aina za neno au maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha Nomino au majina ya vitu, watu au mahali. Maneno haya hutumika katika sentensi pale ambapo nomino haipo, Viwakilishi haviwezi kutumika kwa pamoja na nomino katika sentensi.
Kwa mfano; Yule aliyeandika ubaoni ameandika vizuri
Huyu anapenda kuimba
Wale wanajua sana kukimbia

Aina za Viwakilishi
Viwakilishi vya Nafsi Huru
Viwakilishi vya Nafsi Tegemezi
Viwakilishi Viambata ( vya ngeli)
Viwakilishi vya kuonyesha

(a) Viwakilishi vya nafsi Huru
Aina hii ya viwakilishi hutumika katika ngeli a-wa, hupatikana katika umoja na wingi ambavyo hutegemea nafsi inayohusika
Mfano#000000 solid;margin:15px;width:95%;">
NAFSIUMOJAWINGI
KwanzaMimiyeye
PiliWeweninyi
TatuSisiwao
 
Mfano katika sentensi
 1. Mimi nitakuja….. Sisi Tutakuja
 2. Wewe unafaidika…. Ninyi mnafaidika
 3. Yeye amelala….. wao wamelala

 

(b) Viwakilishi vya Nafsi Tegemezi
Aina hii ya viwakilishi hutumika katika ngeli a-wa na huambatanishwa katika kitenzi. Hutumika kuonyesha nafsi mbalimbali katika umoja na wingi
Mfano#000000 solid;margin:15px;width:95%;">
NAFSIUMOJAWINGI
KwanzaNi_Tu_
PiliU_M_
TatuA_Wa_
 
Mfano Katika sentensi
 1. Nitakuja……. Tutakuja
 2. Utamwona……Mtamwona
 3. Alinieleza……..Walinieleza

 © Viwakilishi Viambata
Aina hii ya viwakilishi huwakilisha ngeli mbalimbali za nomino, pia hutumika katika shina la sentensi kuonyesha umoja au wingi wa nomino inayohusika katika sentensi.
Mfano#000000 solid;margin:15px;width:95%;">[td]
 • mkulima
[/td][td]
 • miti
[/td]
NGELIVIWAKILISHIMFANO KATIKA SENTENSI
aMkulima analima shamba
Wa    Wa-wakulimaWakulima wanalima shamba
U    U- mtiMti umezaa matunda
IMiti imezaa matunda
U     U- UgonjwaUgonjwa umeenea kote
Ya   Ya- magonjwaMagonjwa yameenea kote
Ya    Ya- majiMaji yamemwagika
(d) Viwakilishi vya Kuonyesha
Aina hii ya viwakilishi husimamia Nomino kwa njia ya kuashiria kitu Fulani,
kwa mfano; Yule aliyesoma kwa bidii amefaulu mtihani
                 Hicho wanachokitaka hakipo hapo

3.VIVUMISHI
Hii ni aina ya neno au maneno ambayo hutoa sifa za nomino.
 Kwa mfano; Mzuri, mrefu, mweusi, mwembamba

Aina za Vivumishi
1. Vivumishi vimilikishi
Ni aina ya vivumishi ambavyo huonyesha kuwa kitu Fulani ni mali ya nomino katika sentensi.
Kwa mfano; Amemtuma mtoto wangu
                 Wamewatuma watoto wetu.

2. Vivumishi vya Sifa
Ni aina ya vivumishi ambayo huelezea sifa Fulani za kitu au mtu katika sentensi
Kwa mfano: Raisi hataki viongozi wavivu
                    Viongozi maarufu wamealikwa

3. Vivumishi vya Idadi
Ni aina ya vivumishi ambavyo huonyesha idadi ya vitu katika sentensi.
Mfano; Niletee mikate michache
             Mwanafunzi mmoja amefukuzwa

4. Vivumishi Vionyeshi
Ni aina za vivumishi ambavyo huonyesha ujirani au umbali wa kitu au mtu katika sentensi.
Kwa Mfano; Jengo hili ni langu
                     Mtoto yule ni mtundu

5. Vivumishi Visaidizi
Ni aina za vivumishi ambavyo vinauliza maswali ili kujua uhakika wa kitu au vitu.
Kwa mfano: Kamba ipi imekatika?
                    Umenunua chakula gani?

6. Vivumishi vya Pekee
Ni aina za vivumishi ambavyo huonyesha ziada ya jambo linalotajwa katika sentensi.
Kwa mfano: Sisi sote tulifuzu mtihani
                    Mkuki mwingine umevunjika

7. Vivumishi vya Jina
Ni aina ya vivumishi ambavyo hutoa taarifa zaidi kuhusu nomino nyingine katika sentensi.
Kwa mfano; Mtu mlemavu ana haki pia
                   Wanafunzi wasichana wanajitahidi darasani

8. Vivumishi vya A- unganishi
Ni maneno yanayotumika kutoa taarifa ya jambo au mtu katika sentensi.
Kwa mfano; kiatu cha mtoto kimekatika
                   Jiko la babu bovu

4. VITENZI
Ni neno au maneno yanayoonyesha tendo au matendo katika sentensi.
Kwa mfano: John anapenda kucheza mpira
           Asha anapika vizuri

Aina za Vitenzi
 • Kitenzi Kikuu
 • Kitenzi kisaidizi
 • Kitenzi kishirikishi​

Kitenzi Kikuu

Ni aina ya kitenzi  kinachoelezea kitendo kamili katika sentensi.
Kwa mfano; Mtoto anakunywa uji
                    Mwalimu anafundisha vizuri

Kitenzi kisaidizi
Ni aina ya kitenzi ambacho hutumika pamoja na kitenzi kikuu, hutoa msaada kwa kitenzi kikuu.
 Kwa mfano: Watu walikuwa wanasaidiana kazi
                     Daktari aliyekuwa anamtibu mgonjwa
                      Mwalimu alikuwa anamsaidia mwanafunzi

Kitenzi Kishirikishi
Ni aina ya kitenzi ambacho huweza kuonyesha hali, tabia, au sifa ya mtu au kukanusha pia hali hzo
Kwa mfano; Kesho si sikukuu
                    Mwanao ni mgonjwa
                     Wewe u mwenzetu

5. VIELEZI
Ni aina ya neno au maneno ambayo huelezea matendo yanayofanyika katika sentensi.
Kwa mfano;
Mwalimu anafundisha darasani
Mtoto anacheza shimoni. 

Aina za Vielezi
 1. Vielezi vya namna
 2. Vielezi vya wakati
 3. Vielezi vya idadi
 4. Vielezi vya mahali

 
 1. Vielezi vya Namna

Ni aina za vielezi ambayo huonyesha maneno yanayofafanua namna au jinsi tendo lilivyofanyika.
Kwa Mfano;
Mtoto anatembea polepole
Gari linakimbia kasi barabarani
Aina hii ya vielezi pia imegawanyika katika sehemu tano tofauti ambazo ni
*Vielezi vya namna hali
*Vielezi vya namna vikalili
*Vielezi vya namna halisi
*Vielezi vya namna ala

Vielezi vya namna hali
Aina hii ya vielezi huonyesha jinsi au hali gani kitendo kilifanywa.
Kwa mfano; Walifika salama
                    Sema taratibu

Vielezi vya Namna vikalili
Ni aina ya vielezi ambavyo hurudia rudia neno kama lilivyo.
Kwa mfano; Mtoto mvivu anapenda kutembea tembea mtaani
                     John anapenda kusimama simama barabarani

Vielezi vya namna halisi
Ni aina ya vielezi ambavyo hutuma kuonyesha hali hasa ya utendaji.
Kwa mfano; Tunawapenda sana
                     Nguo haijakauka kabisa

Vielezi vya wakati
Ni aina ya vielezi ambavyo hujibu lini kitendo kilitendeka, kutendwa au lini kitatendwa.
Kwa mfano; Tutaenda kwao kesho asubuhi
                     Asha amenunua matunda leo

Vielezi vya Idadi
Ni aina ya vielezi ambavyo huonyesha kitendo kilichotajwa kilifanyika au kitafanyika mara ngapi,
Kwa mfano; Wameiba tena nguo zetu
                     Tulirudia kusoma mara nyingi
 

Vielezi vya Mahali
Ni aina ya vielezi ambavyo hujibu swali wapi kitendo kilitendeka, mahali gani ambapo kitendo kinachotajwa kilitokea.
Kwa mfano; Wanafunzi wanarudi nyumbani
                     Watoto wanacheza mpira uwanjani

 
6.VIHISISHI
Vihisishi ni aina ya maneno ambayo huibua hisia na mguso katika sentensi. Kuna aina mbalimbali za vihisishi
Baadhi ya vihisishi hivyo ni ;

(a) Vihisishi vya huzuni
Hivi ni aina za vihisishi ambavyo huonyesha hali ya huzuni katika sentensi
Kwa mfano; Loh! Masikini nyumba yangu imebomolewa
                  Yarabi! Yule mtoto amefariki

(b) Vihisishi vya furaha
Hivi ni aina za vihisishi ambavyo huonyesha furaha katika sentensi
Kwa mfano; Oyea! Tumeshindaaa
                     Oyoo! wamerudi na mtoto wetu
 
(c) Vihisishi vya mshtuko
Hivi ni aina za vihisishi ambavyo huonyesha hali ya mshtuko katika sentensi
Kwa mfano; Ha! umekuja lini?
                  Hee!nani amevunja kioo changu


7. VIUNGANISHI
Ni aina ya neno au maneno ambayo huunganisha dhana mbili au zaidi za maana katika sentensi.
Kuna aina mbili za viunganishi
[list=lower-roman]
[*]Viunganishi huru
[*]Viunganishi vitegemezi

 
[list=lower-roman]
[*]Viunganishi Huru

Hii ni aina ya viunganishi ambavyo husimama peke yake katika sentensi moja,Kwa mfano lakini, ila, yani, bali na labda.
[list=lower-roman]
[*]Viunganishi vitegemezi

Ni aina ya viunganishi ambavyo hutokea kama viambishi katika kitenzi/ hutokea katikati ya vipashio vilivyoungwa.
Kwa mfano;
Mtoto aliyeumia amepona
Wanafunzi wanaopiga kelele watachapwa

 

 

 

 
(This post was last modified: 11-06-2017 01:31 PM by MyElimu.)
10-19-2017 06:54 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
Post Icon Uundaji Wa Maneno MyElimu 0 893 12-04-2017 02:22 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon Aina Za Barua MyElimu 0 4,558 02-07-2015 05:05 AM
Last Post: MyElimuUser(s) browsing this thread: 2 Guest(s)