MyElimu
Kwanini Kiswahili Kilisambaa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki? - Printable Version

+- MyElimu (https://myelimu.com)
+-- Forum: GENERAL STUDENTS DISCUSSIONS (https://myelimu.com/forum-general-students-discussions)
+--- Forum: KISWAHILI (https://myelimu.com/forum-kiswahili)
+--- Thread: Kwanini Kiswahili Kilisambaa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki? (/thread-kwanini-kiswahili-kilisambaa-zaidi-tanzania-kuliko-nchi-nyingine-za-afrika-mashariki)

Kwanini Kiswahili Kilisambaa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki? - MyElimu - 02-23-2014

Baada ya uhuru mwaka 1961, lugha ya Kiswahili ilisambaa na kukua zaidi nchini Tanzania kuliko sehemu nyingine Afrika Mashariki. Je, ni sababu zipi zilizopelekea hili?

RE: Kwanini Kiswahili Kilisambaa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki? - Musa - 02-23-2014

Kwa Kenya, kulikuwa na ukabila sana. Watu wa kule hasa wa lugha za Kikuyu na Kijaluo walipenda sana kuongea lugha zao kuliko kiswahili. Waliona kuongea kiswahili ni kijushusha hadhi. Kwa Uganda sina uhakika sana.

RE: Kwanini Kiswahili Kilisambaa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki? - khaleed masoudz - 01-30-2015

 naomba msaada wa uhakiki wa fungate ya Uhuru

RE: Kwanini Kiswahili Kilisambaa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki? - ZAGALO EMANUEL - 01-30-2015

 SABABU ZA KISWAHILI KUENEA TZ
1.Kilitumika kama lugha ya taifa
2.kenya na uganda kulikuwa na ukabila (tribalism)
3.kulianzishwa vyombo vya kukuza lugha ya kiswahili mf.TUKI ,TUMI,TAKILUKI N.K
4. Vyombo vya habari vilitumia kiswahili
5.kilitumika katika shuhughuli za kiserikali mf.bunge

RE: Kwanini Kiswahili Kilisambaa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki? - MyElimu - 02-07-2015

Musa;39 Wrote:Kwa Kenya, kulikuwa na ukabila sana. Watu wa kule hasa wa lugha za Kikuyu na Kijaluo walipenda sana kuongea lugha zao kuliko kiswahili. Waliona kuongea kiswahili ni kijushusha hadhi. Kwa Uganda sina uhakika sana.

Pia, unaweza kusoma kuhusu historia na asili ya Kiswahili hapa http://www.myelimu.com/thread-Historia-Ya-Kiswahili-Na-Asili-Yake

RE: Kwanini Kiswahili Kilisambaa zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki? - williada - 06-11-2015

- ukabila, katika nchi nyingine za afrika mashariki mfano uganda makabila kama baganda na nkole walidhani kuwa wakitumia lugha ya kiswahili lugha zao za kikabila zitapotea, hivyo hivyo hata nchini kenya makabila kama kikuyu nayo yalichangia.

-uwepo wa misitu yenye wanyama kwa mfano simba kwenye misitu ya Tsavo nchini kenya kulifanya kiswahili kutoenea kwani misafara ya wafanyabiashara ambao walikuwa wanaeneza kiswahili walihofia wanyama hao.

-kiswahili kudhaniwa kuwa ni lugha ya kitumwa na kiislamu mfano waganda wengi walikichukia kiswahili kwa kuwa kilitumiwa na waarabu ambapo waliamini kuwa kiswahili kiliimarisha uislamu

-hoja nyingine ni kama ifuatavyo;

_kupingwa na watawala
_kiswahili kuchukuliwa kama lugha duni dhidi ya kiingereza.