MyElimu
Maswali Ya Kiswahili 1 Form 6 - Printable Version

+- MyElimu (https://myelimu.com)
+-- Forum: GENERAL STUDENTS DISCUSSIONS (https://myelimu.com/forum-general-students-discussions)
+--- Forum: KISWAHILI (https://myelimu.com/forum-kiswahili)
+--- Thread: Maswali Ya Kiswahili 1 Form 6 (/thread-maswali-ya-kiswahili-1-form-6)



Maswali Ya Kiswahili 1 Form 6 - MyElimu - 03-23-2015

SEHEMU A: UFAHAMU NA UFUPISHO
 
1. Jibu maswali yote kutoka sehemu hii.
 
Baadhi ya wananchi wakaanza kuamini kwamba huo ndio ulikuwa mtindo wa maisha sasa. Wakaanza kujivunia na kufurahia vitendo vyao vya uovu wakaanza kudhihaki uadilifu na wema.
Wakaanza kukosa huruma
Ubinafsi wa viongozi ukashamiri
Ufisadi (rushwa) ukajichimbia
Uchu wa madaraka ukatawala
Woga wa kufichua wala rushwa ukaigubika nchi.
Ujasiri wa kudai haki za kiraia ukafifia
Mafisadi wakawa vigogo, vilivyoweza kupelekwa mahakama.
Ufisadi hufanya yasiyowezekana, huingilia harakati za uchumi.
Makabwela ndio hukandamizwa zaidi na ufisadi huwasamehe matajiri kulipa kodi, ni kikwazo cha maendeleo.
 
MASWALI:
[list=lower-roman]
[*]Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki.
[*]Mtindo wa maisha sasa ni upi?
[*]Mwandishi analalamika juu ya jambo gani.
[*]Ufisadi unafanya nini?
[*]Unafikiri mwandishi amefanikiwa kufikisha ujumbe.
[/list]
 
 
2. Fupisha habari kwa maneno 30 tu.
 
    SEHEMU B: MATUMIZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
    JIBU MASWALI 2
 
3. Changanua sentensi zifuatazo kwa njia ya matawi, zingatia vigezo vyote viwili
    (a) Watoto wawili wanacheza mpira mkubwa na baba yao anaandika barua fupi.
    (b) Mama mdogo ametusimulia hadhithi ndefu leo jioni
    © Watoto waliadhibiwa walikimbilia nyumbani.
 
4. Eleza ubora na udhaifu wa kuainisha ngeli za nomino kisintaksia.
 
  
     SEHEMU C: UTUNGAJI
5.  Andika mambo muhimu katika uandishi wa ripoti.
 
 
     SEHEMU D: MAENDELEO YA KISWAHILI
6. Ni kwa vipi harakati za ukombozi wa kisiasa nchini Tanzania zilisaidia kukuza na kueneza Kiswahili  kabla ya uhuru.
 
7. Fafanua kwa ufasaha malengo matano (5) ya chama cha Kiswahili cha Afrika mashariki (CHAKAMA).
 
 
SEHEMU E: TAFSIRI NA UKALIMANI
8. (a) Nini maana ya tafsiri?
    (b) Eleza umuhimu wa tafsiri

 


RE: Maswali Ya Kiswahili 1 Form 6 - Guest - 08-19-2016

lula 171/158