12-04-2017, 02:32 PM
0
UHIFADHI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Fasihi simulizi ni aina fasini ambayo huwasilishwa kwa njia yam domo na vitendo na hupokewa kwa kusikilizwa. Fasihi simulizi imegawanyika katika tanzu nne tofauti ambazo ni;
Kila utenzi wa fasihi simulizi una umuhimu wake, kwa pamoja tanzu zote zina umuhimu wake kwa jamii.
Umuhimu wa Fasihi simulizi
Njia zinazotumika Katika Kukuza Fasihi Simulizi
NJIA ZA UHIFADHI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Ubora wake
Udhaifu wake
Ubora wake
Ubora wake.
Udhaifu wake
Ubora wake
Udhaifu wake
Ubora wake
Udhaifu wake
Ubora wake
Udhaifu wake
Umuhimu wa Kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi
Fasihi simulizi ni aina fasini ambayo huwasilishwa kwa njia yam domo na vitendo na hupokewa kwa kusikilizwa. Fasihi simulizi imegawanyika katika tanzu nne tofauti ambazo ni;
- Maigizo
- Semi
- Ushairi
- Hadithi
Kila utenzi wa fasihi simulizi una umuhimu wake, kwa pamoja tanzu zote zina umuhimu wake kwa jamii.
Umuhimu wa Fasihi simulizi
- Hutumika kuelimisha watu, kupitia fasihi simulizi watu hupata maarifa ya kutambua mambo maovu na namna ya kuyakwepa, jamii hujifunza kujitawala, kuzalisha mali na usawa wa demokrasia kupitia kazi za fasihi simulizi.
- Hutumika kutoa mafunzo kuhusu mambo mbalimbali ya historia, dini, siasa, giografia, uchumi na sheria.
- Huwapa watu uwezo wa kuzungumza kwa ufasaha, kuigiza mambo kwa ustadi na kucheza ngoma kwa umaridadi.
- Huhifadhi na kurithisha mambo mbalimbali kuhusu utamaduni kutoka kizazi kimoja kwenda kingine mambo yanayohusu mila na destuli za jamii zao.
- Hutumika kuburudisha na kuleta msisimko wa kimwili na kiakili
- Hudumisha na kukuza lugha, watu hupata misamiati mingi zaidi na miundo ya lugha kupitia kazi za fasihi simulizi
Njia zinazotumika Katika Kukuza Fasihi Simulizi
- Kupitia vikundi mbalimbali vya Sanaa na muziki, vikundi hivi vimeanzishwa ili kuendeleza tanzu mbalimbali za fasihi simulizi mfano wa vikundi hivyo ni vikundi vya Sanaa za maonyesho, vikundi vya taarabu na muziki.
- Wizara ya Elimu kutoa tamko kuwa fasihi simulizi ifundishwe mashuleni kuanzia ngazi ya awali mpaka elimu ya juu.
- Kupitia wizara ya elimu pia imeanzisha vyuo vya Sanaa za maonyesho kwa mfano chuo cha Sanaa cha Bagamoyo, Butimba, Nyegezi, na vingine.
- Vyombo vya habari, hivi navyo vinasaidia kukuza na kueneza fasihi simulizi kupitia vipindi mbalimbali vinavyotangazwa kupitia redio, runinga na kwenye magazeti na majarida, kwa mfano Kuna michezo ya kuigiza
- Kutumia fasihi simulizi kwenye sherehe mbalimbali, kwa mfano kwenye misiba, harusi na mikutano ya siasa hii pia huendeleza na kukuza fasihi simulizi.
NJIA ZA UHIFADHI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
- Kichwani
Ubora wake
- Uwasilishwaji wake unaweza kufanyika wakati wowote bila kuhitaji maandalizi yoyote ya kabla.
- Uhifadhi wake hautumii gharama yoyote.
- Uwasilishwaji wake ni hai, hii ni kwa sababu msimulizi huwa yuko ana kwa ana na hadhira yake kwahiyo anaweza kubadilisha sauti, au miondoko ili kuelezea hisia tofauti tofauti.
Udhaifu wake
- Kuna uwezekano mkubwa wa kazi ya fasihi kupotea pale ambapo msanii wa kazi ya fasihi atapata ugonjwa wa kusahau, au kufariki kazi iliyohifadhiwa kichwani hupotea.
- Ni rahisi kubadilika na kupoteza uhalisia wake wa awali, hii ni kwa sababu msanii anaweza kupoteza baadhi ya matukio ya fasihi kwa kusahau au kuamua kubadilisha ujumbe uliopo.
- Njia ya maandishi
Ubora wake
- Kazi huhifadhiwa katika hali inayoweza kudumu katika kipindi kirefu
- Huweza kufikia hadhira iliyo mbali toka mahali alipo msanii.
- Kupitia njia hii ya kuhifadhi kazi ya fasihi haiwezi kupotea.
- Njia hii hutumiwa na wale wanaojua kusoma tu.
- Hadhira yake ni ya wale wanaojua kusoma tu.
- Wahusika yaani msanii na hadhira yake hawaonani.
- Huhitaji gharama katika kuhifadhi kazi ya fasihi, maandalizi yake huhitaji vitu kama vile peni, karatasi, meza na kiti, vitu hivyo vyote huhitaji fedha ili kuvinunua.
- Hupunguza uhalisia kwa sababu msanii hawezi kutumia matendo katika usimulizi ulio katika njia ya maandishi.
- Njia ya Vinasa sauti
Ubora wake.
- Kazi ya msanii huweza kuwafikia hata hadhira iliyo mbali na mahali alipo msanii au mtunzi wa kazi ya fasihi.
- Kazi ya fasihi huwa haiwezi kupotea wala kuharibika ikiwa itahifadhiwa vizuri.
- Hutunza kumbukumbu kwa muda mrefu
Udhaifu wake
- Hutumia gharama kubwa ili kuweza kurekodi kazi ya fasihi, hii ni kwasababu huhitaji kununua vinasa sauti ambavyo huuzwa kwa bei kubwa.
- Uwasilishwaji wake sio hai hii ni kwasababu wahusika hawaonani wanasikia kwa sauti tu.
- Kazi ya fasihi hubaki mali ya msanii aliyerekodi, mtu mwingine hana ruhusa ya kutumia kazi hiyo bila ruhusa.
- Haiwezi kubadilishwa pale inaporekodiwa hata kama itapitwa na wakati na mazingira yakawa tofauti.
- Njia ya kompyuta
Ubora wake
- Njia hii ni ya uhakika zaidi, kazi zote huhifadhiwa katika komputa na hutolewa pale zinapohitajika.
- Haiwezi kupotea kwa urahisi
Udhaifu wake
- Msanii na hadhira hawawasiliani ana kwa ana, kazi ya fasihi inapunguza uhai wake.
- Hadhira hukosa nafasi ya kuuliza maswali kwa vipengele ambavyo vina utatanishi.
- Lazima msanii awe anajua namna ya kutumia kompyuta.
- Njia hii ni ya gharama kubwa zaidi kulinganisha na njia nyingine.
- Njia ya kanda za video
Ubora wake
- Wasanii na vifaa vinavyotumika huonekana, hivyo huongeza uhai katika kazi ya fasihi.
- Ni njia ya uhakika zaidi na hudumu kwa muda mrefu kama kanda zilizotumika zitahifadhiwa vizuri.
Udhaifu wake
- Njia hii ina gharama kubwa, msanii hutakiwa kununua vifaa kama vile runinga, kanda tupu na kumlipia mpiga picha na atakayerekodi kazi ya fasihi.
- Huwafikia wachache, hufika kwa wale wenye uelewa na uwezo wa kuwa na vifaa kama runinga wengine hawawezi kufikiwa na kazi hizi.
- Hakuna mawasiliano ya ana kwa ana kati ya msanii na hadhira.
- Njia ya makazi
Ubora wake
- Kazi zinapohifadhiwa katika nyumba huweza kubaki salama kwa muda mrefu.
- Msanii hutumia gharama ndogo kuonyesha Sanaa yake kwasababu ya umiliki wa vifaa vya kazi yake.
Udhaifu wake
- Ni rahisi kuharibika kama vyombo vya kazi za fasihi vitahifadhiwa vibaya.
- Ni rahisi vyombo vya kazi ya fasihi kuibiwa kama hakuna ulinzi wa kutosha.
- Ajali kama ya moto na mafuriko huwezi kuteketeza kazi ya Sanaa hiyo.
Umuhimu wa Kuhifadhi kazi za Fasihi Simulizi
- Husaidia kukuza na kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali.
- Fasihi simulizi ni sehemu ya ajira pia kama itatumika kwa lengo la kuingiza fedha.
- Kazi za fasihi simulizi pia huweza kutumika kama vivutio vya utalii
- Huingizia pato taifa kama kutakuwa na njia tofauti za kuhakikisha kazi za fasihi zinatumika ili kuongeza kipato.