0
#DawatiLaMyElimu
Kama MyElimu, lengo letu ni kukusaidia wewe wanafunzi ili uweze kusoma kwa ubora zaidi na kwa urahisi zaidi. Juu ya hilo, ni muhimu kwetu uweze kutumia elimu unayoipata ili uweze kujiendeleza katika karne hii ya 21. Elimu hii haiwezi kubaki kuwa ndani ya darasani tu maana ukimaliza shule nini kinafuata?
Dawati la MyElimu ni segment mpya ya MyElimu ambayo kila mwezi tutakuwa tukikuletea wewe wanafunzi mtu ambaye unaweza kujifunza kutoka kwake mambo mbalimbali, ndani ya shule na nje ya shule kwa ujumla. Awe mfanyabiashara, msanii, mwanafunzi, kijana msajiliamali, na kadhalika - mradi tu anaweza kukufundisha kitu.
Mwezi huu tarehe 13/08 tutakuwa na ndugu Benjamin Fernandes. Benjamin ni mtanzania anayesomea Masters in Business Administration (MBA), Chuo cha Stanford, Marekani na kufanya kazi Bill & Melinda Gates Foundation. Jumamosi atakuwa hapa kwenye #DawatiLaMyElimu atakapokuwa akiongelea namna kijana unaweza kujiendeleza kimaisha bila kujali unapotoka. Ni kuanzia saa 1 mpaka saa 2 jioni. Video itakuwa live. Kama una swali unataka kumuuliza andika swali lako kwenye sehemu ya ya discussion hapo chini nasi tunamfikishia naye atakujibu siku hiyo. Share uwakaribishe na wengine!