Shairi: Tanga Rudi Masomoni
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Shairi: Tanga Rudi Masomoni
MwlMaeda Offline
Teacher
Teacher

Posts: 41
Likes Given: 1
Likes Received: 3 in 3 posts
Joined: Feb 2017
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 3,446.38 points
Country: Tanzania
Post: #1
Shairi: Tanga Rudi Masomoni

0
0
TANGA RUDI MASOMONI.

Keti kitini nikweleze, hukohuko Ngamiani,
Kwa tungo nikuongoze, pakawe sawa kitwani,
Moro usiichokoze, 'takutokea puani,
Tanga rudi masomoni.

Msimbe usimbeze, alikushinda dimbani,
Ngoma yake usiteze, nakushauri mwendani,
Itakuja ikulize, uwe hoi taabani,
Tanga rudi masomoni.

Ninajuwa nikujuze, kutunga ni yangu fani,
Jaribu nikupoteze, upotee duniani,
Ama vipi jisogeze, nikutie darasani,
Tanga rudi masomoni.

Tanga usijikweze, kama kujuwa zamani,
Sasa sinieleze, kuwa ungali fanani,
Mbinu zote umalize, hunifiki abadani,
Tanga rudi masomoni.

Huku Moro sikatize, saiziyo Mombasani,
Kwa hivyo sijitokeze, na kutaka ushindani,
Sitake nikukimbize, kwa bakora hadharani,
Tanga rudi masomoni.

Mja sijiheleleze, na kujitia shidani,
Hata fanya jiongeze, kwa kuenda ugangani,
Tungo ili zipendeze, vema uzame kinani,
Tanga rudi masomoni.

Huko kwenu uwajuze, Kinyonga hawezekani,
Tena wasijiingize, kunifata uwanjani,
Aula wajitulize, waepushe tafarani,
Tanga rudi masomoni.


(JIBU)
TANGA NI CHUO CHA FANI

Rangimoto jitulize, kisha utwae uneni
Goti'chi ulipigize, nikufunze kwa yakini
Elimu ukasambaze, wendapo kwenu nyumbani
Tanga ni chuo cha fani

Nyakangao muulize, Salimu Kibao nani
Na akupe habarize, Jimbi Pera Ridhiwani
Siyo sauti upaze, mithili ya majinuni
Tanga ni chuo cha fani

Jituze mwana jituze, u mchanga kwenye fani
Ngoma hino usicheze, humudu shindo la beni
Ukisema ucheleze, usijejuta mbeleni
Tanga ni chuo cha fani

Ushairi nikujuze, asili yake ni pwani
Kirangacho ukipoze, Morogoro mji duni
Bure sijiangangize, kutaka jipa thamani
Tanga ni chuo cha fani

Unataka uongoze!, eti ushike sukani
Kwa tungo ipi tujuze, nitazamapo sioni
Njoo tukutengeneze, Tanga ndiyo malishoni
Tanga ni chuo fani

La shamba sijipumbaze, huwezi wika mjini
Wagamba nisikatize, hasa kwa kuhofu nini
Nitapita nikujuze, nenda Dodoma chuoni
Tanga ni chuo cha fani

Naacha kupiga zeze, karibu chuo cha fani
Ni Tanga na wilayaze, njoo upate auni
Utunzi tukukoleze, kwa jaala ya Manani
Tanga ni chuo cha faniKaribu: http://www.mwalimuwakiswahili.com
(This post was last modified: 06-10-2017 03:31 PM by MwlMaeda.)
06-08-2017 10:02 AM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Achiever Offline
Junior Member
**
Accelerators

Posts: 5
Likes Given: 2
Likes Received: 1 in 1 posts
Joined: Nov 2016
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 78.84 points
Post: #2
RE: Shairi: Tanga Rudi Masomoni

0
0
Shairi zuri Mwl Maeda. 

Dhamira kuu ni zipi?
(This post was last modified: 06-08-2017 01:12 PM by Achiever.)
06-08-2017 01:11 PM
Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Shairi: Nani Katia Shubiri? MwlMaeda 0 256 07-16-2017 02:57 PM
Last Post: MwlMaedaUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)