Nyimbo Katika Fasihi Simulizi
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Nyimbo Katika Fasihi Simulizi
MwlMaeda Offline
Teacher
Teacher

Posts: 41
Likes Given: 1
Likes Received: 3 in 3 posts
Joined: Feb 2017
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 3,446.38 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Nyimbo Katika Fasihi Simulizi

0
0
Nyimbo ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalum.
Aghalabu nyimbo hutumia ala za muziki kama vile ngoma. Nyimbo zinaweza kuimbwa na mtu mmoja au zaidi.
Wimbo hugawanywa katika beti na mishororo. Nyimbo nyingi huwa na kiitikio au mstari ambao hurudiwa rudiwa.
Sifa za Nyimbo
Hutumia kiimbo au sauti maalum
Huweza kuendamana na ala za muziki
Huimbwa na mtu mmoja au watu wengi; wakati mwingine nyimbo huimbwa kwa kupokezanwa.
Hutumia lugha ya mkato
Hurudiarudia (kukariri) maneno ili kusisitiza ujumbe katika wimbo
Umuhimu wa Nyimbo katika Fasihi Simulizi
Kuburudisha
Kuelimisha, kufunza, kuonya, kuelekeza
Kuliwaza
Kusifia kitu au mtu katika jamii
Kuunganisha jamii
Kudumisha/kuhifadhi tamaduni za jamii
Kukuza talanta na sanaa katika jamii
Hutumika katika mbinu nyingine za fasihi kama vile hadithi
Vipera/Aina za Nyimbo
Kulingana na Muundo:
Mashairi
Maghani
Kulingana na Ujumbe/Maudhui:
Nyimbo za Ndoa

Nyimbo za harusi huimbiwa bwana na bibi harusi kuwapongeza na kuwapa heko kwa kufunga ndoa yao. Aidha nyimbo hizi huwapa wawili hao mawaidha ya kutunza familia na watoto wao ili waishi pamoja.
Nyimbo za Jandoni/Tohara

huimbwa na vijana wanapopashwa tohara. Nyimbo hizi huonyesha ushujaa, na kuashiria kutoka kwamba anayetahiriwa amekuwa mtu mzima sasa.
Hodiya/Wawe

Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa na watu wanapofanya kazi ili kuwatia bidii wafanye kazi bila kuhisi machofu.
Kimai

Nyimbo za Mabaharia - Hizi ni nyimbo za wanabahari wanaposafiri baharini.
Nyimbo za Mazishi/Huzuni/Simanzi

Hizi ni nyimbo za kuliwaza na kuwapa pole walioachwa na marehemu. Nyimbo hizi huwapa matumaini waombolezaji.
Nyimbo za Kidini

Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa kumsifia Mungu, kuomba au kutoa mafunzo ya kidini.
Nyimbo za Kisiasa

Hizi ni nyimbo za kuwasifia viongozi wa kisiasa
Nyimbo za Kizalendo

Nyimbo za huonyesha uzalendo kwa kusifia taifa/nchi
Nyimbo za Mapenzi

Katika nyimbo za mapenzi, mwimbaji huimba kwa kumsifia mpenzi wake hasa kwa urembo na tabia zake.
(This post was last modified: 06-09-2017 12:28 PM by MwlMaeda.)
06-09-2017 12:23 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
Post Icon Fasihi Kwa Ujumla MyElimu 0 496 09-14-2017 01:19 PM
Last Post: MyElimu
  Kunani Katika Maisha Yangu Na Baada Ya Miaka Hamsini MwlMaeda 0 152 06-11-2017 05:54 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Udhibiti Wa Kazi Za Fasihi Kwa Ufupi MwlMaeda 0 265 06-08-2017 07:09 PM
Last Post: MwlMaeda
  Madoido Katika Fasihi MwlMaeda 0 193 06-07-2017 10:57 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Sifa Pambanuzi Za Kifani Za Utendi Andishi Wa Kiswahili Zinavyojitokeza Katika Utenzi MwlMaeda 2 400 06-07-2017 01:38 PM
Last Post: MwlMaeda
Post Icon Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mbalimbali. Damian 3 1,057 05-23-2017 02:16 PM
Last Post: kemmyqlyon
Lightbulb Tanzu na Vipera Vya Fasihi Simulizi Given 1 24,438 12-21-2015 11:07 AM
Last Post: SUSAN MACHARIA
Post Icon Fani Na Maudhui Katika Fasihi MyElimu 0 6,844 09-12-2014 02:17 PM
Last Post: MyElimu
Post Icon Siti Binti Saadi - Mtunzi mkongwe wa Fasihi ya Kiswahili Given 0 2,107 02-20-2014 11:40 PM
Last Post: GivenUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)