Melodrama/tanzia-ramsa/futuhi/komedia (comedy/kichekesho)
How to register and join MyElimu CLICK HERE

Post Reply 
 
Thread Rating:
  • 0 Votes - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Melodrama/tanzia-ramsa/futuhi/komedia (comedy/kichekesho)
MwlMaeda Offline
Teacher
Teacher

Posts: 41
Likes Given: 1
Likes Received: 3 in 3 posts
Joined: Feb 2017
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 3,446.38 points
Country: Tanzania
Post: #1
Post Icon Melodrama/tanzia-ramsa/futuhi/komedia (comedy/kichekesho)

0
0
MELODRAMA
Katika zama za urasimi, aina hii ilitumiwa kuelezea aina ya drama au tamthiliya iliyokuwa na matumizi mengi ya uimbaji au nyimbo (melos). Kwa hiyo, melodrama ni dhana inayotumiwa kuelezea aina ya tamthiliya ambayo imetawaliwa na uimbaji wa nyimbo.
Melodrama inafanana sana na tanzia ingawa mara nyingi nguli wa melodrama humalizika na ushindi, matokeo yake yanasisimua sana na mwendo wa msuko wake huwa ni wa haraka haraka zaidi. Wahusika wake huvutia na kufurahisha lakini hawana sifa za kishujaa.
Dhamira ya melodrama huzungukia mvutano kati ya wema na uovu au ubaya. Miishio ya tamthiliya hizi haina sifa ya mtakasohisia kama ilivyo na tanzia bali huwa ni aina ya ushindi wa mhusika mwema. Mfano mzuri ni ‘The Begger’s Opera’ iliyotungwa na mwanatamthiliya wa Kiingereza John Gay kunako 1728.


TANZIA-RAMSA
Ni tamthiliya inayochanganya vipengele vya tanzia na ramsa, hutumiwa sawa na tamthiliya za kibwege - hii ni tamthiliya ambayo inaonyesha kwamba kicheko au furaha ndiyo jibu pekee la maisha kwa watu ambao hawana imani na maisha ambayo kwayo misingi thabiti ya maisha imeondolewa. Mfano tamthiliya ya Amezidi ya S.A Mohamedi
Tanzia-ramsa ni tamthilia ambayo huonyesha mabadiliko ya aina fulani yanayogeuza mwelekeo wa matukio ya kitanzia na kuufanya kuwa tofauti au wa kufurahisha. Hali hii inaweza kupatikana kwa kuwepo kwa hasidi au mui anayetubu na kuyajutia makosa au msimamo wake au kuwepo kwa mandhari ya kiulimbwende.
Kimsingi, tanzia-ramsa ni tanzia inayoishia kwa furaha. Kinyume chake ni futuhi zimbwe. Dhana hii inaakisi kwa kiasi kikubwa baadhi ya mitazamo ya kidhanaishi ya fasihi ambapo ushujaa na tanzia havijitokezi katika hali ya kawaida kama vilivyozoeleka.
Hali hii inadhihirika katika tamthiliya kama vile ‘The Cherry Orchard’ (Anton Chekhov, 1904), ‘The Winter’s Tale’ (William Shakespeare, 1611).


Shujaa wa kiramsa
• Si lazima awe mtu maalum/mbabe au shujaa, anaweza kuwa mtu wa kawaida
• Mhusika wa ramsa lazima awe mtu wa wastani chini ya wastani, awe ni mtu ambaye hatarajiwi kujitokeza na mtu wa nasaba duni na matendo yake yawe ya ucheshi
• Ni lazima awe mtu ambaye akifanikiwa wasomaji au watazamaji watafurahi
Uhusika katika ramsa
• Ramsa inawahusu watu wa kawaida kuliko ilivyo tanzia
• Inawahusu watu wa kipato cha kati na cha chini
• Dhamira zote huelekezwa kwa watu wa kipato cha chini na duni. Mfano walalahoi
SIFA ZA RAMSA
• Sharti ivutie akili na siyo hisia
• Ni lazima kuwa na matendo bila kufikiria hii itapelekea msomaji au mtazamaji kujua kwamba wahusika hawa hawana akili
• Lazima iwe na hali ya utu (ikitukumbusha ubinadamu wetu)
• Sharti iwe na mila na desturi ambazo hadhira inazifahamu toka katika jamii yake
• Hadhira isiogope au kupata uchungu kwa sababu hii sio lengo lengo la ramsa
• Wahusika wa ramsa hujaribu kuepuka vikwazo ambavyo vimewekwa
• Inaonyesha haja ya kuikomboa nafsi Mfano wa ramsa ni kama vile Mfalme Juha.


FUTUHI/KOMEDIA (COMEDY)
Futuhi au komedia ni utungo ambao unachekesha na kuchangamsha. Tamthiliya ya aina hii inaweza kusawiria picha halisi katika maisha kwa undani ikitumia dhihaka na kejeli kwa kuchekesha. Futuhi huficha ukali wa masuto kadri inavyoendelea kuburudisha hadhira yake.
Futuhi hulenga kurekebisha tabia zinazozidhihaki au zinazozicheka. Kusema futuhi inafurahisha haina maana kuwa dhamira yake haina uzito, kwani huzungumzia masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa njia ya kuchekesha. Futuhi huweza kuwa na sifa zinazotofautiana – jambo ambalo hutumiwa kama kigezo cha kuainisha aina mbalimbali. Lakini vyovyote iwavyo, futuhi hujikwepesha na masuala ya kutia hofu au kushtua.
Athari ya futuhi (kuchekesha) hutokana na matendo, mienendo ya wahusika na hitilafu au ila za kuingiliana kwa kiusemi. Futuhi huwa na viwango mbalimbali vya kuchekesha.
Kwanza, kuna kiwango hafifu (duni) ambacho huhusishwa na futuhi ya chini. Kuna baadhi ya kazi ambapo kiwango cha kuchekesha huwa kigumu kutambulikana na huhitaji utambuzi mpevu. Hii ni sifa ya aina ya futuhi iitwayo Futuhi ya Juu.
Aina zingine ni pamoja na, futuhi ya kikanivali, kitashtiti, maadili, mawazo, ucheshi na zimbwe. Mifano mizuri ya futuhi ni ‘Aliyeonja Pepo’(Topan, F.), ‘Usaliti Mjini’ (Imbuga, F.), Twelfth Night (Shakespeare, W.), Importance of Being Earnest (Wilde Oscar), Mkaguzi Mkuu wa Serikali (Gogol, Nikolai), The Lion and the Jewel (Soyinka, W.) na ‘Masaibu ya Ndugu Jero’ (Soyinka, W.).


KICHEKESHO/FUTUHI/KOMEDIA (COMEDY)
Futuhi au komedia ni utungo ambao unachekesha na kuchangamsha. Tamthiliya ya aina hii inaweza kusawiria picha yakini katika maisha kwa undani ikitumia dhihaka na kejeli kwa kuchekesha. Futuhi huficha ukali wa masuto kadri inavyoendelea kuburudisha hadhira yake.
Futuhi hulenga kurekebisha tabia inazozidhihaki au inazozicheka. Kusema futuhi inafurahisha haina maana kuwa dhamira yake haina uzito. Futuhi huzungumzia masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa njia ya kuchekesha. Futuhi huweza kuwa na sifa zinazotofautiana – jambo ambalo hutumiwa kama kigezo cha kuainisha aina mbalimbali. Lakini vyovyote iwavyo, futuhi hujikwepesha na masuala ya kutia hofu au kushtua.
Athari ya futuhi (kuchekesha) hutokana na matendo, mienendo ya wahusika na hitilafu au ila za kuingiliana kwa kiusemi. Futuhi huwa na viwango mbalimbali vya kuchekesha.
Kwanza, kuna kiwango hafifu (duni) ambacho huhusishwa na futuhi ya chini. Kuna baadhi ya kazi ambapo kiwango cha kuchekesha huwa kigumu kutambulikana na huhitaji utambuzi mpevu. Hii ni sifa ya aina ya futuhi iitwayo Futuhi ya Juu.
Aina zingine ni pamoja na, futuhi ya kikanivali, kitashtiti, maadili, mawazo, ucheshi na zimbwe. Mifano mizuri ya futuhi ni ‘Aliyeonja Pepo’(Topan, F.), ‘Usaliti Mjini’ (Imbuga, F.), Twelfth Night (Shakespeare, W.), Importance of Being Earnest (Wilde Oscar), Mkaguzi Mkuu wa Serikali (Gogol, Nikolai), The Lion and the Jewel (Soyinka, W.) na ‘Masaibu ya Ndugu Jero’ (Soyinka, W.).
06-07-2017 02:40 PM
Visit this user's website Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Musa Offline
Gold Student
Gold
Accelerators

Posts: 22
Likes Given: 2
Likes Received: 4 in 4 posts
Joined: Feb 2014
Reputation: 0
Friend:  Add as Friend

Points: 153.45 points
Post: #2
RE: Melodrama/tanzia-ramsa/futuhi/komedia (comedy/kichekesho)

0
0
Asante sana aisee. Unatusaidia sana.
06-07-2017 03:08 PM
Find all posts by this user Like Post Quote this message in a reply
Post Reply 


You may also like these discussions:
Thread: Author Replies: Views: Last Post
  Mfano Wa Kichekesho MwlMaeda 0 391 07-09-2017 08:49 AM
Last Post: MwlMaeda
  Mfano Wa Kichekesho MwlMaeda 0 176 07-08-2017 11:27 AM
Last Post: MwlMaedaUser(s) browsing this thread: 1 Guest(s)