02-25-2014, 07:51 PM
Madaraja Yaliyotumika Kwenye CSEE 2013
|
02-25-2014, 11:21 PM
0 Madaraja haya yamewezesha wanafunzi wengi kuonekana wamefaulu kwa division nzuri ingawa kama wangepimwa kwa viwango vya zamani wasingepata division walizopata sasa, nadhani katika kusaidia kuboresha elimu si vema kushusha viwango vya ufaulu ili wengi waonekane wamefanya vizuri, bali ni kuhakikisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ikiwemo maslahi ya wlaimu yanaboreshwa. Haya ndiyo maoni yangu.
09-08-2014, 07:57 AM
0 (02-25-2014, 11:21 PM)Masozi Wrote: Madaraja haya yamewezesha wanafunzi wengi kuonekana wamefaulu kwa division nzuri ingawa kama wangepimwa kwa viwango vya zamani wasingepata division walizopata sasa Mkuu hii point hii wengi sana huitumia pasipo kuelewa ! Hizi grade zimewakandamiza sana wanafunzi ! Mfano Daraja 'C' ata kama zingetumika grade za zamani bado lingekuwa linaanzia points 41 ambayo kwa mwaka jana ilihesabika ikiwa na thamani ya 3, Lakini sasa thaman yake ni 4 B plain (nayo ingebaki kuwa ni ''C'' ) haya ona sasa aliyepata alama hizi B, B, B, B, C, C, C kwa mwaka huu ana points 24 lakini zingetumika grade za mwaka jana hizo 'B' zingekuwa 'C' na 'C' zingebaki kuwa 'C' kwahiyo angekuwa na C, C, C, C, C, C, C ambapo angepata points 21 huoni jinsi zilivyo waumiza baadhi ya wanafunzi mkuu ? Quote: nadhani katika kusaidia kuboresha elimu si vema kushusha viwango vya ufaulu ili wengi waonekane wamefanya vizuri, bali ni kuhakikisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ikiwemo maslahi ya wlaimu yanaboreshwa. Haya ndiyo maoni yangu.
Chozi Lishikalo Moyo!
|
Users browsing this thread: |
2 Guest(s) |